Walimu na wanafunzi wa Mbezi High School wamekuwa mstari wa mbele katika uchangiaji wa damu kwa ajili ya kusaidia akiba ya damu ya taifa ambapo kila mara wamekuwa wakijitolea kuchangia damu.
Mkuu wa shule hiyo Said Amran anasema kuwa ni kawaida kwa walimu na wanafunzi wake kuchangia damu kwa vile wanatambua umuhimu wa kufanya hivyo ili kuwasaidia Watanzania wenzao.
Mkuu huyo wa shule alisema hayo wakati wa zoezi la uchangiaji damu mbali liliendeshwa na Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki shuleni hapo hivi karibuni.
Zaidi ya wanafunzi 20 walichangia damu hiyo wakati wa zoezi hilo ambalo lilifanywa na wataalum wa kutoa damu akiwe mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Judith Chale.
No comments:
Post a Comment