Bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia imepata pigo kwa kufiwa na Meneja Mauzo wake, Bonny Kasyanju aliyefariki dunia usiku wa kuamia leo Julai 11 baada ya kuugua kwa muda wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa Msemaji wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, Bonny alikukuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ini na figo
ambapo alilazwa katika hospitali ya Lugalo, jijini Dar es Salaam hadi mauti ilipomkuta.
"Bado mipango ya mazishi inaendelea kufanyika, baada kukamilika tutatoa taarifa zaidi, lakini ni kwamba kwa sasa tuna msiba wa kufiwa na Meneja Mauzo wetu Bonny," alisema Mkinga.
Hata hivyo, Msemaji huyo hakufafanua zaidi kama bendi hiyo itasimamisha maonyesho ili kuomboleza msiba kwa madai kwamba hadi ratiba ya mazishi itakapotolewa na familia ya marehemu.
No comments:
Post a Comment