Meneja wa bendi hiyo, Doborah Nyangi ndiye amesema hayo na kuongeza kuwa wanenguaji hao wanatosha na kwamba Kalunde haina mpango wa kuongeza wengine zaidi ya hao wawili.
"Tuna wanenguaji makini wanaoshirikiana kwa karibu katika kazi, wanapendana na wanajua kufanya kazi ya muziki, hivyo hatuoni sababu yoyopte ya kuongeza wengine, hawa wanatutosha na tunajivuna kuwa nao," alisema Deborah.
Alisema kwa wingi wa wanenguaji kwenye bendi kama yao haina umuhimu wowote hasa kwa kuzingatia kwamba huwa inapiga muziki kwenye kumbi tulivu ambazo hazihjitaji kuwa na kundi kubwa la wanenguaji.
"Wingi wa wanenguaji nao nio tatizo, kwani uzoefu unaonyesha kwamba wakiwa wengi hawawezi kufanya kazi kwa kushirikiana, kila mmoja atataka kujiona kuwa ni bora kuliko mwingine," alisema.
Alisema bendi hiyo sasa inajiandaa kuwa ya kimataifa, hivyo idadi tya wanamuziki waliopo inatosha na kwamba inaweza kuongeza wengine pale inapobidi lakini sio kwa upande wa wanenguaji.
Bendi hiyo imekuwa kambini kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku ikiandaa nyimbo mpya na nyingine za kukopi huku ikiendelea na maonyesho kama kawaida kwenye ambazo imekuwa ikitoa burudani.
Nyimbo mpya zilizokambilishwa kwenye kambi ya bendi hiyo ni 'Masumbuko', 'Sisee' na 'Fungua' na 'Ulinipendea Nini' ambazo baadhi yake zimeanza kusikika kwenye maonyesho ya bendi hiyo.
Miongoni mwa kumbi ambazo Kalunde imekuwa ikitoa burudani ni Triniti ambako bendi hiyo hufanya vitu vyake kila Jumatano na Ijumaa kisha Jumamosi huwa Joevic na kumalizia wikiendi katika ukumbi wa Giraffe Ocean View, Mbezi Beach.
No comments:
Post a Comment