Watu wanaowaajiri wafanyakazi wa majumbani, wametakiwa kuacha kuwaita watumishi hao kwa majina mabaya, kwa madai kwamba kufanya hivyo ni kushusha hadhi na utu wao.
Hayo yalisemwa na wawezeshaji wa semina ya Waajiri Makini iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la KIWOHEDE linalohudumia Afya na Maendeleo ya Wanawake na watoto ambalo kifupi linajulikana kama kiota.
Pamoja na hayo, wametakiwa kuepuka kuwaajiri wafanyakazi wenye umri chini ya miaka 17 kutokana na ukweli kwamba ajira kwa watoto wadogo kosa kulingana na sheria za kimataifa kuhusu ajira za watoto.
Kwa mujibu wa Edda Kawala na Stella Mwambenja ambao wote wanatoka KIWOHEDE, tabia ya waajiri kuwaita majina mabaya watumishi wao na kuwanyanyasa ama kuwabagua ni jambo baya kwani linashusha hadhi na utu wao.
Wawezeshaji hao walisema ni wajibu waajiri kuishi vizuri na watumishi wao na kuwafanya kama sehemu ya familia zao badala ya kuwabagua na kunyanyapaa, kitu ambacho sio ubinadamu.
No comments:
Post a Comment